Meneja wa Young Dee aelezea jina la ‘Paka Rapa’ na sababu za kukataa show hivi karibuni

Meneja wa Young Dee ‘Maxmilian’ amesema hali ya rapa huyo imeimarika na anaendelea vizuri hivyo watu watarajie kazi nzuri kutoka kwake.
Max amesema “Sasa namfananisha Young Dee kama ‘Paka’ kwa hiyo kwa wale watu wanaomuita Paka rapa huyo naona hawakosei kwa kuwa Young Dee ameimarika na kuwa mkali zaidi ya watu walivyomzoea awali”.
Hata hivyo Max alisema watu wasimuelewe vibaya anapomkatalia msanii huyo kufanya show na kwamba haimaanishi kuwa wanadharau kiasi cha pesa wanachopewa, bali walikuwa wanajipanga zaidi na kuhakikisha Young Dee anakuwa mpya.
Pia Max amepiga mkwara juu ya ujio mpya wa msanii huyo na kusema mashabiki zake wajipange kwani akiachia wimbo utakuwa zaidi ya ‘Hands Up!’ kwa kuwa kwa sasa Young Dee ni zaidi ya mtoto wake kwa hiyo nimemuandaa vyema.

Post a Comment

0 Comments